Tawi la baraza hilo katika jimbo la Arizona liliitisha mkutano na waandishi wa habari jana Ijumaa ili kupinga kitendo cha maadui wa Uislamu cha kukusanyika mbele ya msikiti wa Phoenix wa jimbo hilo.
Mkutano huo na waandishi wa habari umeitishwa na Waislamu hao ili kujibu kundi la wapanda pikipiki wenye silaha waliokusanyika mbele ya msikiti huo.
Jon Ritzheimer mwanajeshi wa zamani wa Marekani mwenye chuki kubwa dhidi ya Uislamu na ambaye ameandaa maandamano hayo ya kupinga Uislamu aliiambia televisheni ya CNN siku ya Alkhamisi kwamba wamejiandaa kutangaza waziwazi upinzani wao dhidi ya Uislamu.
Waislamu wa jimbo la Arizona wamewataka maafisa usalama wa Marekani walinde usalama wao hususan kutoka na Waislamu hao kupokea barua za vitisho zinazotishia maisha yao.