IQNA

Mwakilishi wa Iran ashika nafasi ya pili mashindano ya Qur'ani ya kimataifa Russia

11:38 - September 21, 2014
Habari ID: 1452134
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameshika nafasi ya pili katika mashindano ya Qur'ani ya kimataifa nchini Russia.

Mahdi Ghulamnejad ambaye alishika nafasi ya nne katika mashindano ya Qur'ani ya taifa, alishiriki katika kitengo cha qiraa na kushinda nafasi ya pili katika mashindano ya kimataifa ya Russia.
Ripoti zinasema kuwa, Mahdi Ghulamnejad alichuana na maqari kutoka nchi 38 katika mashindano hayo. Mashindano hayo yalifanyika jana Jumamosi yakisimamiwa na Baraza la Mamufti la Russia na chini ya himaya ya serikali ya Moscow hususan Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.
Saad al Ghamidi ambaye ni miongoni mwa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani mzaliwa wa Dammam, Saudi Arabia alikuwa miongoni mwa wageni makhsusi wa mashindano hayo.
Sambamba na mashindano hayo ya 15 ya kimataifa ya Qur'ani ya Russia, Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kilitayarisha maonyesho ya Qur'ani kandokando ya shughuli hiyo.  AIR    1451998

captcha