IQNA

Ramadhani katika Qur’an/1

Qur’ani Inasemaje kuhusu Mwezi wa Ramadhani

9:43 - March 14, 2024
Habari ID: 3478504
IQNA – Qur’ani Tukufu inataja neno Ramadhani mara moja na hilo lipo katika Aya ya 185 ya Surah Al-Baqarah.

Katika aya hii, kuna maelezo kuhusu mwezi mtukufu, ikiwa ni pamoja na moja ya kuteremshwa kwa Quran.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 185 ya Sura Al-Baqarah: “Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.”

Kwa mujibu wa aya hii, Ramadhani ni mwezi ambao Qur’ani Tukufu iliteremshwa ndani yake, na unapowadia mwezi huu, kila Mwislamue ambaye amefikia umri wa Takleef (9 kwa wasichana na 15 kwa wavulana - ambao wanatakiwa kufuata faradhi za kidini) lazima afunge.

Kuna maoni tofauti kuhusu jinsi Qur’ani ilivyoteremshwa katika mwezi huu. Wengine wanasema iliteremshwa mara moja huko Bait al-Mamour au kiliteremshwa kwenye anga ya dunia katika Usiku wa Qadr na kisha kuteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) hatua kwa hatua. Mtazamo mwingine unashikilia kuwa mwanzo wa kuteremshwa Qur’anI ulikuwa ni Usiku wa Qadr ndani ya Ramadhani.

Ingawa neno Ramadhani lenyewe limetajwa ndani ya Qur’anI mara moja tu, kuna aya nyingi ambazo funga ya Ramadhani inazungumzwa bila kutaja Ramadhani.

Kwa mfano, kuna Aya za 183 na 184 za Surah Al-Baqarah:

“Enyi mlio amini, mmelazimishwa kufunga kama walivyolazimishwa watu wa kabla yenu, ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu. (Aya ya 183)

“(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.”(Aya  184)

Mwenyez Mungu anaepusha makundi matatu ya kufunga Mwezi wa Ramadahni: wagonjwa, walio safarini, na wazee. Kundi la kwanza na la pili lazima wafidie wanapopata afya au safari yao imekwisha. Lakini kundi la mwisho (wazee) wanatakiwa tu kulipa Kaffara (fidia ya hisani), ambayo ni bei ya gramu 750 za ngano au vitu vingine kama hivyo.

3487526

Habari zinazohusiana
captcha