IQNA

Kadhia ya Palestina

Mahathir Mohammad akosoa udhaifu wan chi za Kiislamu kuhusu Gaza

15:25 - November 29, 2023
Habari ID: 3477964
TEHRAN (IQNA)- Kutokana na udharura na haja ya kuongezwa na kuimarishwa umoja na mshikamano baina ya wapenda uhuru na wapigania haki hususan nchi za Kiislamu katika kuilaani Israel, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Mahathir Mohammad amesema: “Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, ili nchi za Kiislamu zimshinde Mzayuni na adui wao wa pamoja hazina njia nyingine ghairi ya kudumisha umoja, kuimarisha msingi wa ulinzi na nguvu za kijeshi.

 

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Mahathir Mohamad, alieleza kuwa nchi nyingi za Kiislamu hazina jeshi imara, na kwa msingi huo, tunaona jinsi Waislamu wanavyokandamizwa na wasiokuwa Waislamu. Kwa mujibu wa Mahathir Muhammad ni kuwa, kwa kuzingatia msisitizo wa Quran na mafundisho ya Kiislamu, ni lazima tuwe tayari na kuujiimarisha kwa zana ili kuweza kulinda na kutetea taifa la Kiislamu.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo mkongwe wa Malaysia, ikiwa nchi za Kiislamu haziwezi kusimama kidete, zenye nguvu na zikiwa zimeshikana mikono mbele ya maadui zao wa pamoja, ni lazima tukubali ukweli mchungu ambao ni kwamba, hatuwezi kufikiria mustakabali mwema wa kukombolewa Palestina. Kwa msingio huo, operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ilionyesha kuwa, Wazayuni ni dhaifu na ni mithili ya debe tupu na ikiwa nguvu ya ulimwengu wa Kiislamu itaimarishwa, ni rahisi kuiondoa Israel kwenye ramani ya kijiografia ya eneo hilo na hivyo kuifuta katika mgongo wa ardhi.

Tokea Oktoba saba, Utawala haramu wa Israel, ukisaidiwa na nchi za Magharibi hususan Marekani na Uingereza, umeua zaidi ya Wapalestina elfu 15 , wengi wao wakiwa wanawake na watoto, katika mashambulizi ya siku ya 49 dhidi ya watu wa Gaza. Wapalestina wengine zaidi ya milioni moja wamelazimiia kuwa wakimbizi na maelfu ya nyumba, shule, mahospitali na miundombinu ya Gaza imeharibiwa kikamilifu.  

4184799

Habari zinazohusiana
captcha