IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

OIC yahimizwa kubuni mkakati kukabiliana na Kukua kwa chuki dhidi ya Uislamu

15:43 - July 08, 2023
Habari ID: 3477253
ISLAMABAD (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imehimizwa kubuni mikakati ya kukabiliana na chuki inayoongezeka dhidi ya Uislamu duniani kote.

 

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alitoa wito wa mkakati kama huo katika mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa OIC Hissein Ibrahim Taha siku ya Ijumaa.

Amesema stratijia hiyo inapaswa kuratibiwa na kueleweka kwa kina na yenye lengo la kuongeza uelewa wa dunia kuhusu mtazamo Uislamu na kwamba inapaswa kujenga kizuizi cha kisheria na kisiasa dhidi ya kushamiri matukio ya chuki dhidi ya Waislamu na chuki dhidi ya Uislamu.

Kiongozi huyo wa Pakistan alionyesha kulaani vikali vitendo hivi vya makusudi na vya uchochezi ambavyo vimeumiza hisia za Waislamu kote ulimwenguni, akimaanisha kuchomwa moto kwa Qur'ani Tukufu nchini Uswidi mwishoni mwa mwezi Juni.

Shehbaz alisisitiza kuwa kuchafuliwa kwa dini, shakhsia za kidini zinazoheshimika, Maandiko Matakatifu na alama haziwezi kuachwa kwa kisingizio cha kujitakia cha uhuru wa kujieleza na kuandamana.

Alishukuru nafasi ya Katibu Mkuu wa OIC katika kueleza wasiwasi na matakwa ya Umma wa Kiislamu kuhusu mielekeo na matukio haya ya chuki dhidi ya Uislamu.

Huku akikaribisha kuitishwa kwa mjadala wa dharura katika Baraza la Haki za Kibinadamu lenye makao yake makuu mjini Geneva kuhusu suala hilo, Sharif alisisitiza kuwa OIC lazima iwasilishe suala hilo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na katika vikao na vyombo vingine vinavyohusika ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa OIC alitangaza msimamo sawa Pakistan kuhusu matukio ya kuchukiza ya kuvunjiwa hadharani Qur'ani Tukufu. Alisisitiza dhamira thabiti ya OIC ya kukabiliana na janga la kisasa la chuki dhidi ya Uislamu.

3484252

captcha