IQNA

Jinai za Israel

Makundi ya Palestina yapata ushindi Jenin, Israel yaambulia patupu

16:53 - July 06, 2023
Habari ID: 3477247
TEHRAN (IQNA) - Makundi ya muqawama yamewapongeza wananchi wa Palestina kwa kupata ushindi mkubwa wa kufanikiwa kuzima uvamizi na mashambulizi ya jeshi katili la Israel dhidi ya Wapalestina katika mji wa Jenin, kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amewapongeza Wapalestina kwa ushindi huo ambao umeudhalilisha na kuutweza utawala wa Kizayuni. 

Operesheni hizo za wanamuqawama na mujahidina wa Kipalestina zimehitimisha uvamizi na hujuma za kinyama za jeshi la Israel na kuwalazimisha wanajeshi makatili wa Israel kuondoka kwa idhilali kwenye mji huo.

Ismail Haniya amebainisha kuwa, "Tunamwambia adui Mzayuni kwamba, siku za kufanya jinai dhidi ya taifa la Palestina pasi na kulipa gharama zimekwisha." 

Naye  Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina, Ziyad al-Nakhalah amepongeza ushindi huo wa taifa la palestina mkabala wa Wazayuni na kueleza kuwa, ushindi huo wenye izza umetokana na operesheni za Brigedi za Jenin kwa kushirikiana na Brigedi za al-Quds.

Amesisitiza kuwa, mujahidina wa Kipalestina hawapaswi kuwa na shaka wala kigugumizi katika vita na adui Mzayuni kwani adui huyo muda si mrefu ataangamia.

Jeshi la utawala wa Kizayuni tangu  Jumatatu lilifanya mashambulizi ya kinyama ya anga na kuushambulia mji wa Jenin huko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, na kuua shahidi Wapalestina 12 na kujeruhi makumi ya wengine. Wazayuni walilazimika kusitisha ukatili wao huo siku ya Jumanne usiku.

Operesheni dhidi ya Jenin haijakuwa na matunda yoyote kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel pia vimekiri suala hilo. Gazeti la Kizayuni la Yediot Aharonot limeandika kwamba nguvu na uwezo wa harakati za ukombozi wa Palestina katika kambi ya Jenin umelishangaza jeshi la Israel na inaonekana kuwa harakati ya Jihad Islami imewekeza katika kuimarisha miundo mbinu ya mapambano katika eneo hilo.

Gazeti la Kizayuni la Ha'aretz pia limeutahadharisha utawala wa Tel Aviv kuhusu matokeo ya uvamizi dhidi ya Jenin na kuandika kuwa: "Operesheni ya hivi sasa ya Jenin na picha zilizochapishwa zinaonyesha kutibuka kizazi kipya cha Wapalestina ambacho hakitatafakari kuhusu chochoce isipokuwa mapambano na muqawama."

Kwa kuzingatia uchambuzi huo wa magazeti ya Kizayuni, inaweza kusemwa kwamba operesheni dhidi ya Jenin sio tu kwamba haikumaliza mgogoro wa ndani katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabvu, bali tishio dhidi ya utawala huu pia limeongezeka.

3484238

captcha