IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

OIC yatoa wito kwa vyombo vya habari kupambana na chuki dhidi ya Uislamu

16:38 - July 06, 2023
Habari ID: 3477246
MAKKA (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Jumatano ilitoa wito kwa nchi wanachama wake kufadhili utayarishaji wa vipindi vya radio, televisheni na vyombo vingine vya habari kwa lengo la kupambana na chuki dhidi ya Uislamu.

Hatua hiyo inalenga "kufafanua na kuimarisha kanuni za uvumilivu za Uislamu zinazotaka kuishi pamoja, kuvumiliana, na kuheshimu wengine na kuachana na ghasia, kutovumiliana na chuki," Mkurugenzi wa Idara ya Habari Wajdi Ali Sindi aliambia mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Mashirika ya Utangazaji ya OIC inayojulikana kama OSBU.
Mkutano huo ulijadili mbinu za kukabiliana na kuvunjiwa heshima kwa matukufu ya kidini katika vyombo vya habari kufuatia kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani Tukufu nchini Sweden wiki iliyopita.
Sindi alisema OIC inashirikiana na washirika wake "kuongeza uelewa wa matumizi ya kuwajibika ya uhuru wa kujieleza katika vyombo vya habari, na kuanzisha mifumo ya kitaifa ya kuwajibika kwa vyombo vya habari vinavyoendelea kueneza kauli za chuki na kutovumiliana, na kutekeleza mkakati wa vyombo vya habari vya OIC ili kupambana na chuki dhidi ya Uislamu."

3484229

captcha