Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Issa Ahmad Mohammad Hassan Al-Kandari ametoa taarifa na kusema misikiti yote Kuwait ina ruhusa kuanzisha tena darsa za Qur’ani, harakati za kiutamaduni na mafunzo ya kidini kwa kuhudhuria ana kwa ana.
Misikiti ya Kuwait ilisimamisha shughuli zote zaidi ya miezi 18 iliyopita kutokana na janga la COVID-19.
Waziri Al Kandari amesema misikiti itatakiwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19 ikiwa ni pamoja na na kuvaa barakoa na kutokaribiana.
Misikiti imefunguliwa tena kikamilifu nchini Kuwait baada ya serikali ya nchi hiyo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi kufanikiwa kudhibiti maambukizi ya COVID-19. Nchi zingine za Kiarabu ambazo zimechukua maamuzi kama hayo ya Kuwait ni pamoja na Qatar, Algeria na Misri.