IQNA

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah

Lebanon inakaribia kupata ushindi mkubwa dhidi ya magaidi

10:12 - August 25, 2017
Habari ID: 3471141
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu harakati ya Hizbullah cha nchini Lebanon amesema ushindi mwingine mkubwa umekaribia nchini humo kwani katika kipindi kifupi kijacho, magaidi wote wa ISIS au Daesh watafurushwa katika mpaka mzima wa Lebanon na Syria na usalama kurejea eneo hilo.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo Alhamisi usiku kwa njia ya televisheni mjini Beirut wakati alipokuwa anatoa ufafanuzi kuhusu opereseheni ya pamoja ya jeshi la Syria na wanamapambano wa Hizbullah wa Lebanon katika milima ya Qalamoun ya mpakani mwa nchi hizo mbili.

Aidha amewaambia viongozi wa genge la kigaidi la ISIS kuwa ushindi wa jeshi la Syria, la Lebanon na vikosi vya Hizbullah katika operesheni ya kuikomboa milima ya mpakani mwa nchi hizo mbili ni jambo lisilozuilika tena, hivyo wasijidanganye kudhani kuwa wataweza kuzuia ushindi huo.

Kiongozi wa Hizbullah amebaini wazi kuwa, mapambano katika milima ya mpakani mwa nchi hiyo na Syria yataendelea hadi yatakapoangamizwa kikamilifu magenge ya kigaidi.

Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, operesheni hiyo inayofanyika kwa maelewano kamili na jeshi la Lebanon imefanikiwa kuwafurusha magaidi wa ISIS katika maeneo yaliyokusudiwa Syria na Lebanon.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon aidha amesema, tangu wiki iliyopita, wanamapbano wa Hizbullah kwa kushirikiana na jeshi la Syria walianzisha opereseheni ya kuwafurusha magaidi wa ISIS katika maeneo ya mpaka wa nchi hizo mbili na kuongeza kuwa, licha ya kundi la ISIS kutumia raia kama ngao ya vita lakini jeshi la Lebanon na lile la Syria pamoja na vikosi vya Hizbullah vimepata ushindi mkubwa kwenye opereseheni hiyo.

3634204

captcha