IQNA

Maonyesho ya Sanaa za Kiislamu, Lagos Nigeria

16:43 - September 02, 2015
Habari ID: 3357526
Maonyesho ya Sanaa za Kiislamu yenye anuani ya 'Mbegu ya Amani' yanafanyia Lagos nchini Nigeria katika Jumba la Makumbusho ya Kitaifa.

Kwa mujibu wa jarida la 'This Day Live', maonyesho hayo yaliyoanza Jumatatu hii yataendelea hadi Septemba 6 ambapo kutakuwa na maonyesho ya athari 40 za kazi za Ridwan Oshinowo ambaye anafanya kazi katika shirika la HALLAL Art Grallemeo. Maonyesho hayo yanafanyika kwa himaya ya Waqfu wa IBEJI na Jukwaa la Kiislamu la Elimu ambalo hujihusisha zaidi na harakati za misaada kwa wanafunzi wasiojiweza sambamba na kueneza maisha ya maelewano baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu.
Sherehe za ufunguzi zimehudhuriwa Sultan wa Sokoto, Alhaji Abubakar Sa'ad pamoja na wanadiplomasia wa nchi kadhaa.
Waislamu ni takribani asilimia 60 ya wakaazi  wote milioni 140 wa Nigeria.../mh

3354626

captcha