IQNA

Mashekhe Waislamu Nairobi waanzisha 'Msafara wa Amani'

14:26 - August 29, 2015
Habari ID: 3353707
Nchini Kenya Jumuiya ya Mashekhe Waislamu Nairobi NMC wameanzisha msafara wa kuhubiri dhidi ugaidi na misimamo mikali miongoni mwa vijana Waislamu.

Msafara huo utatembelea kaunti zote 47 nchini humo ili kueneza ujumbe wa amani , mapenzi, maelewano na kuishi pamoja kwa maelewano baina ya Waislamu na jamii zingine nchini humo. Kwa mujibu wa gazeti la Standard, msafara huo ulizinduliwa Alhamisi katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi ambapo kiongoni wa NMC Ibrahim Abdullahi amesema hujuma za kigaidi zimewagawanya Wakenya kwa misingi ya kidini na hivyo msafara huo ambao pia utaanzia Mombasa unalenga kuonyesha kuwa Waislamu wanapinga ugaidi.
"Uislamu ni dini ya amani na ile anayeiharibia dini hii jina, hazingatti mafundisho halisi na ya kweli ya dini hii tukufu," amesema.
Abdullahi amelaani vitendo vya kigaidi na kusema makundi ya kigaidi yanatumia dini kuwagawa Wakenya kwa misingi ya kidini na wakati huo huo kupelekea Waislamu walengwe na kubaguliwa.
Aidha ameelezea wasiwsi wake kuhusu kuendelea kutoweka vijana Waislamu ambao wanatumiwa na watu wenye misimamo mikali kueneza ugaidi.
Uzinduzi wa msafara huo umehudhuriwa pia na wawakilishi wa Wakristo ambao wamesema watashrikiana kwa karibu na NMC.../mh

3353539

captcha