IQNA

Slovakia yawazuia wahajiri Waislamu kuingia nchini humo

15:55 - August 22, 2015
Habari ID: 3350005
Slovakia imetangaza kuwa itawakubali tu wahajiri Wakristo wakati wa kuwachukua wakimbizi kutoka Syria.

Nchi hiyo inatazamiwa kupokea wakimbizi 200 kutoka kambi za Uturuki, Italia na Ugiriki kwa mujibu wa sheria mpya ya Umoja wa Ulaya ya kugawana wakimbizi 40,000 waliowasili barani humo kutoka Afrika na Mashariki ya Kati.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Slovakia imesema haitawaruhusi wakimbizi Waislamukuingia nchini humo kwa madai kuwa eti nchi hiyo haina misikiti hivyo itakuwa vigumu Waislamu kuishi hapo.
Huku hayo yakijiri Umoja wa Mataifa ulionya kuhusu vitendo vya ubaguzi dhidi ya wahajiri wanaoingia barani Ulaya. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni baada ya serikali ya Slovakia kutangaza kuwa, itawapokea wahajiri wa Kikristo tu nchini humo. Joel Millman, msemaji wa umoja huo amesema kuwa, UN inapinga ubaguzi wa kijinsia, wa kidini au wa kikabila dhidi ya wahajiri. Akiashiria ripoti zinazotolewa juu ya kuwepo vipendo vya aina hiyo nchini Slovakia na Hungary, Joel alisema kuwa, ubaguzi dhidi ya wahajiri ni tatizo la ulimwengu mzima na kwamba, Umoja wa Mataifa unapinga aina yoyote ya mienendo hiyo kwa taifa lolote lile.../mh

3349633

captcha