IQNA

Idadi ya Misikiti duniani kufika milioni 4 mwaka 2019

21:02 - July 29, 2015
Habari ID: 3336897
Idadi ya misikiti duniani inakadiriwa kuongezeka na kufika takribani milioni nne ifikapo mwaka 2019.

Hayo ni kwa mujibu  wa ripoti ya Shirika la Deloitte na Kituo cha Ustawi wa Uchumi wa Kiislamu Dubai , idadi ya misikiti duniani sasa ni milioni 3.6 na idadi hiyo ikiongozeka kwa kasi ya sasa itafika milioni 3.85 mwaka 2019.
Ripoti hiyo imesema misikiti mipya inayojengwa katika nchi mbali mbali bado haiwezi kukidhi mahitaji ya Waislamu wanaoongezeka kwa kasi kubwa duniani. Ripoti hiyo imesema kuna uhaba mkubwa wa misikiti barani Ulaya kwani kuna ongezeko kubwa la Waislamu barani humo kutokana na kusilimu raia wengi wa bara hilo.
Ufaransa ni kati ya nchi ambazo zinahitaji misikiti mingi mipya. Dalil Bubakr, mkuu wa Baraza la Kiislamu la Ufaransa amesema nchi hiyo ina Waislamu milioni saba lakini idadi ya misikiti ni 2,200 pekee.
Nchini Uingereza kuna misikiti 1,000 kwa ajili ya Waislamu milioni mbili nchini humo ambao ni asilimia tano ya watu wote nchini humo. India ndio nchi yenye idadi kubwa zaidi ya misikiti duniani. Nchi hiyo ina misikiti 300,000, idadi ambayo inazidi ile ya nchi yoyote ile duniani.../mh

3336374

captcha