IQNA

OIC yataka Umoja wa Mataifa uzuie hujuma za Israel Al Aqsa

12:38 - July 27, 2015
Habari ID: 3335772
Shirika la Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC limetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhuckua hatua hatua za kivitendo kuzuia hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa.

Katibu Mkuu wa OIC Iyad Ameen Madani ametoa taarifa na kusema utawala wa Israel unapaswa kubebeshwa lawama kuhusu kuendelea hujuma dhidi ya Msikiti.  Amesema vitendo vya Israel vitapelekea kuibuka vita vya kidini, misimamo mikali na ukosefu wa uthabiti katika eneo.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuwawekea vizingiti Wapalestina wanaoenda kuswali katika msikiti wa al Aqsa. Uchunguzi umebaini kuwa asilimia 90 ya Wapalestina wanaamini kuwa Israel inatekeleza njama za kubomoa Msikiti wa Al Aqsa na mahala pake kujenga hekalu la Kiyahudi.../mh

 

Kishikizo: MADANI oic israel kizayuni
captcha