IQNA

Mwanamke Mwislamu Marekani alipwa fidia ya $25,000 kwa ajili ya Hijabu

13:11 - July 25, 2015
Habari ID: 3334845
Bi.Samantha Elauf aliyenyimwa kazi na shirika la Abercrombie & Fitch nchini Marekani kwa sababu alivaa vazi la staha la Hijabu wakati wa mahojiano ya kutafuta kazi sasa amelipwa fidia kufuatia amri ya mahakama.

Shirika hilo la kuuza nguo limekubali kumlipa Bi. Elauf dola za Kimarekani 25,000  baada ya kupatikana na hatia ya kumyima kazi kwa ajili ya vazi lake la Hijabu.
Mwezi uliopita Mahakama ya Rufaa Marekani ilipiga kura 8-1 na kuamua kuwa shirika la Abercrombie & Fitch lilikiuka haki za  kidini ya Elauf kwa kukataa kumuajiri mwaka 2008 kama mfanaykazi katika  duka la nguzo za watoto la Abercrombie Kids huko Tulsa, Oklahoma.
Shirika hilo mbali na kumlipa fidia Elauf limetakiwa pia kulipa gharama za mahakama zilizokadiriwa kuwa $ 18,983.
Kubagua mfanyakakazi kwa msingi wa kidini ni kinyume cha sheria za kifederali nchini Marekani isipokuwa pale itakapohisika kutakuwa na usumbufu mkubwa kwa mfanyakazi.
Pamoja na kuwa Elauf alipata pointi nyingi katika mahojiano lakini alinyimwa kwazi kwa ajili tu alikuwa amevaa mtandio.../mh

3332184

captcha