IQNA

Wapalestina Ukanda wa Ghaza wapinga ubaguzi wa Israel

21:54 - March 03, 2015
Habari ID: 2921399
Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wameandaa hafla kadhaa kwa mnasaba wa wiki ya kupinga ubaguzi unaotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakazi wa Ghaza wameandaa hafla hizo pamoja na kuwa eneo hilo liliharibiwa sana katika hujuma ya miezi kadhaa iliyopita ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Makumi ya miji duniani inafanya marasimu ya kuadhimisha wiki ya 11 ya ubaguzi wa Israel (IAW) katika juhudi za kuzidisha ufahamu kuhusu ukatili unaofanywa na utawala wa Tel Aviv dhidi ya raia wa Palestina. Wiki ya ubaguzi ni silsila ya matukio ya kimataifa ya kila mwaka yanayojumuisha maandamano, mihadhara, maonyesho ya kitamaduni, uonyeshaji wa filamu, maonyesho ya media anuai sambamba na kufanyika shughuli mbalimbali zinazohusiana na ususiaji unaoongezeka na kampeni ya vikwazo dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni. Tangu kuanza kwake katika mji wa Toronto nchini Canada mwaka 2005, matukio hayo ya kila mwaka ambayo yamekuwa yakifanyika mwezi Februari au Machi, hivi sasa yameenea katika miji isiyopungua 200 duniani. Mikutano na mihadhara ilifanyika jana nchini Afrika Kusini na katika eneo la Ukanda wa Ghaza lililo chini ya mzingiro wa kiuchumi wa Israel, ambapo raia wa Palestina walifanya shughuli mbalimbali katika kuadhimisha wiki ya ubaguzi wa Israel.../mh

2920256

captcha