IQNA

Waislamu 14,000 walazimishwa kuondoka Myanmar

21:38 - November 09, 2014
Habari ID: 1471524
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamearifu kuwa, Waislamu wa jamii ya Rohingya wamelazimishwa kuondoka nchini Myanmar katika wiki 3 ziliopita kutokana mpango mpya wa serikali uliozusha mjadala.

Kwa mujibu wa mpango huo unaoitwa Rakhine Action Plan, zaidi ya Waislamu milioni moja wa kabila la Rohingya watafukuzwa nchini humo iwapo watashindwa kuthibitisha kwamba familia zao zimeishi nchini Myanmar kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita. Waislamu hao wa Mynamar pia wanaweza kufungwa jela kwa muda usiojulikana kwa mujibu wa mpango huo wa kibaguzi, ambao unawataka wakubali kupangwa tena kimakabila na kuandikishwa kuwa ni Wabengali au kufungwa jela.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yameitaka jamii ya kimataifa iishinikize serikali ya Myanmar kufuta mpango huo na kuutaja kuwa hauna maana yoyote zaidi ya kuthibitisha kuendelea ubaguzi wa rangi.

Jamii ya Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakikabiliwa na ubaguzi, manyanyaso na kupuuzwa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1948. Katika miaka miwli iliyopita Waislamu wengi wa Myanmar wameuawa huku zaidi ya laki na nusu wakikimbia makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali.../mh

1470872

captcha