Mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Habari wa nchi za Kiislamu (ICIM) umefanyika Jumatano hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na Is’haq Jahangiri Makamu wa Kwanza wa Rais na Katibu Mkuu wa OIC.
2014 Dec 04 , 00:42
Ayatullahil Udhma Nasser Makarem Shirazi mmoja wa maulama na wanazuoni wakubwa nchini Iran amekosoa vikali siasa za kindumakuwili za baadhi ya madola ya Mashariki ya Kati kuhusiana na matukio ya eneo hili likiwemo suala la kundi la kigaidi la Daesh.
2014 Dec 02 , 18:35
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali shambulizi la kigaidi kwenye Msikiti Mkuu wa Kano, Nigeria jana Ijumaa, ambalo limeripotiwa kupelekeka kuuawa watu zaidi ya 120 na kuwajeruhi wanaokisiwa kuwa mamia ya wengine.
2014 Nov 29 , 20:04
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kujihisi kuwa na majukumu ya kibinadamu, kuwa na maarifa ya kumjua Mwenyezi Mungu na busuri, ni misingi mikuu ya fikra za kimantiki za jeshi la kujitolea la Basiji.
2014 Nov 28 , 06:10
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumanne mjini Tehran ameonana na maulamaa, wanavyuoni, wasomi na wageni walioshiriki kwenye Kongamano la Kimataifa la Mirengo ya Kitakfiri kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu na kulitaja suala la kuzuka upya makundi ya kitakfiri katika miaka ya hivi karibuni kuwa ni tatizo lililopandikizwa na mabeberu katika ulimwengu wa Kiislamu.
2014 Nov 26 , 10:28
Kongamano la Kimataifa kuhusiana na Tishio la Makundi ya Kitakfiri na Yenye Kufurutu Ada limeanza leo katika mji mtukufu wa Qum hapa nchini Iran kwa kuhudhuriwa na masheikh na maulamaa kutoka nchi mbalimbali duniani.
2014 Nov 23 , 11:50
Bunge la Uhispania na Rais wa Slevonia wameunga mkono suala la kutambuliwa rasmi dola la Palestina. Hatua hii inakuja katika wimbi la uungaji mkono wa dola la Palestina.
2014 Nov 19 , 23:09
Kamati ya Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya imetangaza vikwazo vipya dhidi ya utawala wa Israel kutokana na hatua za utawala huo za kuvuruga usalama wa Baitul Maqdis na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
2014 Nov 19 , 23:03
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametahadharisha kuhusu njama za adui zenye lengo za kuudhihirisha Uislamu kuwa ni tishio.
2014 Nov 18 , 17:54
Imebainika kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ulikuwa umepanga kumuua Kiongozi wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah katika Siku ya Ashura, Novemba 4.
2014 Nov 15 , 11:23
Mabunge ya Uhispania na Ufaransa yamepanga kupigia kura azimio la kulitambua taifa la Palestina, hatua ambayo imekuwa ikichukuliwa ma nchi kadhaa za Ulaya.
2014 Nov 14 , 20:42
Kufuatia kuongezeka na kuenea malalamiko ya Wapalestina katika mji wa Quds (Baitul Maqdis) unaokaliwa kwa mabavu, Ghaza na Ukingo wa Magharibi hivi sasa Wapalestina wanaoishi katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu, yaani Israel, nao pia wameandamana.
2014 Nov 10 , 14:03
Ghasia na machafuko mapya yamezuka kati ya askari wa utawala wa kizayuni wa Israel na waandamanaji wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel baada ya utawala huo kufunga Msikiti mtukufu wa al Aqsa.
2014 Nov 06 , 10:21