Vyombo vya usalama vya Iraq vimeripoti kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Imam Sadiq (as) nchini humo ametekwa nyara katika mkoa wa Karkuk.
2011 Nov 06 , 10:13
Khatibu wa swala ya Ijuma ya Bahrain amesema kuwa watu wanaochochea fitina za kimadhehebu kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni wanapuuza dini, ubinadamu na matukufu yote.
2011 Nov 05 , 21:12
Ayatullahil Udhma Khamenei:
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo Jumatano asubuhi ameonana na maelfu ya wanafunzi na wanachuo hapa mjini Tehran katika muda huu wa kukaribia tarehe 13 Aban (yaani Novemba 4) ambayo nchini Iran inahesabiwa kuwa ni siku ya mwanafunzi na siku ya taifa ya kupambana na ubeberu duniani.
2011 Nov 02 , 20:56
Tamasha la Kiislamu la 'Idul Adh'ha Mjini' linaendelea mjini Marseille kwa udhamini wa Muungano wa Familia za Waislamu.
2011 Nov 02 , 17:21
Kikao cha kitaalamu kilichojadili nafasi ya wanawake katika mapinduzi ya Misri kimefanyika leo tarehe Mosi Disemba mjini Tehran kwa hima ya Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu.
2011 Nov 02 , 02:51
Shughuli ya kuwakumbuka askari Waislamu wa Ufaransa waliouawa katika Vita vya Kwanza vya Dunia itafanyika tarehe 10 Novemba katika mji wa Lyon.
2011 Oct 31 , 10:32
Waziri Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki amesema kuwa mpango wa kuanzisha mfumo wa federali katika mkoa wa Salahuddin una lengo la kuigawa Iraq.
2011 Oct 31 , 10:31
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amemkaribisha ofisini kwake Kiongozi wa eneo la Kurdistan la Iraq Bwana Mas'ud Barzani na ujumbe anaoandamana nao hapa nchini.
2011 Oct 30 , 15:49
Kamanda wa jeshi la polisi katika mkoa wa Karbala nchini Iraq amesema kuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida katika mkoa huo Khamis al Kartani ametiwa nguni.
2011 Oct 30 , 11:57
Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel mapema leo zimeshambulia Ukanda Gaza.
2011 Oct 30 , 11:29
Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo mjini Tehran amewataka watawala wa White House nchini Marekani wajifunze kutoka katika historia na kuacha udanganyifu wa kisiasa. Ayatullah Jannati amesisitiza kuwa, walimwengu wameanza kupambana na mfumo wa kibepari.
2011 Oct 29 , 18:01
Imam na khatibu wa msikiti wa Aal al Rasul (saw) katika mkoa wenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia wa Ihsaa huko mashariki mwa Saudi Arabia amesema kuwa inasikitisha kuona kwamba mwenendo wa kuwavunjia heshima Waislamu wa Kishia katika mimbari bado unaendela.
2011 Oct 26 , 16:45
Wanazuoni wa Kituo cha Kiislamu kinachofungamana na chuo cha kidini cha al-Azhar cha nchini Misri wametoa fatuwa wakiharamisha ufungaji ndoa na vibaraka pamoja na watu waliokuwa karibu na utawala wa dikteta Hosni Mubarak kutokana na ufisadi wa kisiasa na vilevile hiana ya watu hao dhidi ya maslahi ya kitaifa ya Misri.
2011 Oct 24 , 15:31