Mashindano ya 53 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia yatafunguliwa rasmi Jumamosi ijayo katika sherehe itakayohudhuriwa na mfalme na nchi hiyo na mke wake katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
2011 Jul 13 , 18:12
Semina ya Ijue Qur'ani Tukufu itafanyika katika siku za tarehe 23 na 29 Julai katika kituo cha Waislamu wa madhehebu ya Shia Ithnaashari mjini Dubai.
2011 Jul 12 , 15:46
Msahafu wa kitaifa wa Mauritania ulipewa jina la Shanqit utazinduliwa rasmi kufikia mwishoni mwaka huu wa 2011.
2011 Jul 12 , 14:56
Washindi wa mashindano ya Qur'ani ya Al Maher nchini Uganda wametunukiwa zawadi Julai 11 katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.
2011 Jul 12 , 14:28
Warsha kuhusu falaki zitafanyika katika Maonyesho ya 19 ya Kimatafa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ambayo hufanyika katika mwezi mtukufu wa Qur'ani.
2011 Jul 12 , 14:22
Shirika la Tabligh ya Kiislamu la Bilal (Bilal Muslim Mission) nchini Kenya limetoa wito kwa Waislamu wanaojiweza nchini humo kutoa misaada kwa wale wasiojiweza katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2011 Jul 12 , 12:35
Wiki ya Nne ya Mafunzo ya Qur’ani Tukufu ilianza jana nchini Algeria chini ya anwani ya Nafasi ya Mazungumzo ya Kiqur’ani katika Kuwazindua Wanadamu.
2011 Jul 10 , 23:21
Taasisi ya Kiilsamu ya al Houda ya Ufaransa imewataka Waislamu wa mji wa Gennevilliers kufanya maandamano Ijumaa ijayo kupiga kitendo cha kufungwa kituo cha ibada cha Waislamu wa mji huo.
2011 Jul 10 , 23:19
Mashindano ya kitaifa ya kiraa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya wanawake nchini Brunei yalimalizika jana. Mashindano hayo yamefanyika kwa lengo la kuwaenzi wanawake wateule.
2011 Jul 10 , 18:58
Mahufadh wa Qur'ani kutoka nchi 70 wametangaza kuwa tayari kushiriki katika mashidano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Misri yatakayofanyika Agosti 19, sawia na 19 mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.
2011 Jul 10 , 16:00
Tamasha ya pili ya Qur'ani Tukufu itafanyika tarehe 7 Agosti mwaka huu katika mji wa Ottawa nchini Canada.
2011 Jul 09 , 17:32
Hafidhi wa Qur'ani wa Tunisia:
Baada ya kuondolewa madarakani utawala wa Bin Ali nchini Tunisia harakati za Qur'ani zimepata umuhimu zaidi nchini kote na kumeanzishwa taasisi nyingi katika uwanja huo.
2011 Jul 09 , 16:44
Kitengo cha wanawake katika Taasisi ya Kuhifadhi Qur’ani mjini Jeddah Saudi Arabia kimetangaza kwamba kitaanda kozi ya kuhifadhi Qur’ani maalumu kwa wanawake.
2011 Jul 09 , 10:24