Al-Azhar imezindua vituo 538 vya masomo ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya watoto katika vijiji na maeneo ya mbali ya nchi hiyo ya Kiarabu, na kufanya jumla ya vituo hivyo kufikia 1045.
Watoto wanaovutiwa na kozi za Qur'ani Tukufu za kusoma au kuhifadhi wanaweza kufanya mtihani wa kuingia na kuanza kujifunza kwenye vituo hivyo.
Sheikh Abdelmuneim Fuad, Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar , anasema mipango inaendelea kutatua matatizo ya vituo hivyo na kuvipa teknolojia mpya.
Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.
Shughuli za Qur'ani hufanyika kwa wingi sana Misri ambapo wasomaji maarufu zaidi wa Qur'ani Tukufu duniani ni kutoka Misri.
4108377