IQNA

Ubaguzi wa rangi Marekani

9 Wauawa katika hujuma dhidi ya kanisa la Wamarekani Weusi

6:05 - June 19, 2015
Habari ID: 3315932
Watu 9 wameuawa kwenye shambulizi la kibaguzi dhidi ya kanisa moja la Wamarekani Weusi usiku wa kuamkia leo katika jimbo la Carolina Kusini.

Kati ya waliouawa ni Seneta wa Baraza la wawakilishi kwenye jimbo hilo, Clementa Pinckney na dada yake. Pinckney ni miongoni mwa wanasiasa wachache wenye asili ya Kiafrika ambaye amekuwa kwenye baraza la wawakilishi tangu mwaka 1997. Kijana Mmarekani mweupe aliyekuwa na bunduki alivamia kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal Church Jumatano usiku na kuanza kufyatua risasi ovyo na kuua watu 9 papo hapo. Polisi jimboni hapo wamesema shambulizi hilo linatokana na chuki na ubaguzi dhidi ya watu weusi na kwamba mshambulizji ameshakamatwa.

Ubaguzi wa rangi nchini Marekani umeshtadi mno katika miaka ya hivi karibuni ambapo polisi weupe wamekuwa wakiwaua kiholela vijana wa Kimarekani wenye asili ya Afrika. Maandamano ya mara kwa mara yamekuwa yakifanyika kupinga ubaguzi huo wa rangi katika nchi inayojinadi kuwa kinara wa haki, uadilifu na usawa katika jamii.

3315852

Kishikizo: marekani ubaguzi afrika
captcha