Sheikh Mkuu wa al Azhar nchini Misri Ahmad al Tayyib ametoa taarifa akilaani kitendo cha kundi la kigaidi la Daesh cha kumchoma moto akiwa hai rubani Moaz al-Kassasbeh wa Jordan. Amekitaja kitendo hicho kuwa ni cha kigaidi na kishetani.
2015 Feb 04 , 17:04
Makamu wa zamani wa rais wa Misri Mohammad El Baradei Ijumaa ametuma aya ya Qur’ani kupitia mtandao wa kijamii wa twitter kujibu hujuma za kigaidi zilizotekelezwa na wanamgambo katika eneo la Sinai nchini Misri ambapo watu 30 waliuawa.
2015 Jan 31 , 17:03
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, amesema kuwa, harakati hiyo imejiandaa kikamilifu kukabiliana kwa aina yoyote na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na kwamba haiwezekani utawala huo uue watu kisha uishi salama.
2015 Jan 31 , 16:11
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maafa makubwa yanayofanywa na makundi ya kigaidi kama lile la Boko Haram yanaathiri na kuumiza sana dhamira za wanadamu kote dunia.
2015 Jan 27 , 20:20
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kadhia ya Palestina ndiyo yenye umuhimu mkubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama kidete hadi pale malengo ya Palestina yatakapotimia na hapana shaka kuwa vijana watashuhudia siku hiyo.
2015 Jan 27 , 16:23
Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu duniani wanaendelea kulaani kitendo cha hivi karibuni cha jarida moja la Ufaransa la Charlie Hebdo kuchora vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtumu Mtukufu wa Uislamu, Mohammad SAW.
2015 Jan 26 , 11:11
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini akisema kuwa, matukio ya hivi karibuni nchini Ufaransa na matukio yanayoshabihiana na hilo katika baadhi ya nchi za Magharibi yamemlazimisha azungumze nao moja kwa moja.
2015 Jan 22 , 20:32
Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kamanda wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni yataendelea hadi Quds Tukufu ikombolewe.
2015 Jan 22 , 00:30
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kujiepusha na ugaidi, misimamo mikali na utumiaji mabavu kwa kisingizio cha kulinda dini.
2015 Jan 22 , 00:27
Kongamano la Tano la Kimataifa la “Ghaza, Nembo ya Muqawama (mapambano)” lilifanyika hapa Tehran siku ya Jumapili kwa minajili ya kukumbuka na kuadhimisha siku ya ushindi mkubwa wa wanamapambano wa Palestina katika vita vya siku 22 vya Ghaza vilivyoanza mwishoni mwa mwaka 2008 na kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2009.
2015 Jan 19 , 13:56
Wanachama wasiopungua sita wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah nchini Lebanon wameuawa, baada ya helikopta ya utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia kwa makombora maeneo ya milima ya Golan ndani ya ardhi ya Syria.
2015 Jan 19 , 13:54
Waislamu wa kila pembe duniani wameendelea kulaani vikali kitendo cha jarida linalochapishwa Ufaransa la Charlie Hebdo cha kuchapisha tena picha za vikatuni vya kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW.
2015 Jan 18 , 06:40
Kansela wa Ujerumani Bi Angela Markel amesema kuwa, Waislamu wanaoishi nchini humo ni .miongoni mwa jamii ya Wajerumani
2015 Jan 13 , 17:19