Shekhe Mkuu wa Chuo Kikuu cha kidini cha al Azhar nchini Misri amepinga hatua ya wahubiri wa Kiwahabi na Kisalafi ya kutumia kauli isiyofaa ya ‘Rafidh’ kuwataja Wapenzi wa Ahul Bayt wa Mtume SAW.
2015 Jul 04 , 19:25
Zaidi ya Waislamu 150 wameuawa katika mashambulio ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram kaskazini mwa Nigeria.
2015 Jul 03 , 23:26
Jumuiya ya Waislamu wa Kishia Tanzania, AfroShia Muslim Community, inapanga maandamano ya amani kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds kwa lengo la kulaani jinai dhidi ya Wapalestina na pia kuunga mkono jitihada za amani duniani.
2015 Jul 03 , 01:14
Waislamu duniani wametakiwa wasisahau kadhia ya kupigania ukombozi wa Palestina katika kipindi hiki ambapo wengi wanajishughulisha na tatizo sugu la ugaidi na jinai zinazotekelezwa na kundi la kigaidi na kitakifiri la Daesh au ISIS.
2015 Jul 01 , 19:31
Wanamaji wa jeshi la utawala haramu wa Israel wameiteka nyara meli ya misaada ya Sweden iliyokuwa imebeba misaada ya Wapalestina walio katika eneo linalozingirwa la Ukanda wa Ghaza.
2015 Jun 29 , 16:07
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hujuma ya hivi karibuni ya kigaidi dhidi ya msikiti nchini Kuwait.
2015 Jun 28 , 19:12
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa wale wanaotaka kuficha uadui wa Marekani na baadhi ya vibaraka wao kwa kutumia nyenzo za kipropaganda ni wasaliti wa taifa na nchi ya Iran.
2015 Jun 28 , 18:55
Serikali ya Tunisia imeamua kufunga misikiti 80 inayoendeshwa nje ya udhibiti wake, siku moja baada ya kutokea shambulio la kigaidi na kupelekea makumi ya watu kuuawa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
2015 Jun 28 , 05:09
Waislamu takribani 350,000 wameshiriki katika sala ya Ijumaa ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika msikiti wa Al Aqsa katika Quds Tukufu.
2015 Jun 27 , 17:31
Wabahrain wamefanya maandamano ya kulaani na kukosoa siasa hizo za ukandamizaji na utiwaji nguvuni wapinzani hasa Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wifaq.
2015 Jun 27 , 16:21
Watu wasiopungua 25wameuawa kufuatia hujuma ya kigaidi iliyolenga msikiti wa Imam Sadiq AS katika mji wa Kuwait.
2015 Jun 26 , 22:42
Magaidi wa kundi la Kitakfiri la Daesh au ISIS wamebomoa makaburi mawili ya kale ya Mawalii wa Allah SWT katika mji wa kihistoria wa Palmyra mkoani Homs nchini Syria.
2015 Jun 24 , 17:02
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusiana na mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 kwamba, vikwazo vya kiuchumi, kifedha na kibenki dhidi ya taifa hili vinapaswa kuondolewa mara moja wakati wa kutiwa saini makubaliano na kwamba, kuondolewa vikwazo hivyo, hakupaswi kufungamanishwa na utekelezaji wa ahadi za Tehran.
2015 Jun 24 , 14:01