Kutokana na ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu huko Malawi, Waislamu nchini humo wameanzisha kampeni ya kuwashawishi wafuasi wa dini nyinginezo kuzingatia msingi wa ‘kuishi pamoja kwa amani’ ili kuzuia uwezekano wa kuibuka malumbano ya kidini katika nchi hiyo ya kusini wa Afrika.
2014 Dec 18 , 12:57
Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh. Takribani miaka 1375 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) Imam Hussein bin Ali (AS) akiwa na watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria.
2014 Dec 13 , 17:40
Waislamu nchini Kenya wanataka vyombo vya habari nchini humo vifanye mabadiliko ya kimsingi kuhusu namna vinavyo tangaza habari kuhusu ugaidi na kuonya kuwa mfumo wa sasa usio wa kitaalamu wa kutangaza habari ni chanzo cha chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
2014 Dec 11 , 11:42
Kiongozi wa Jumuiya ya Jamaatud Dawa nchini Pakistna Hafidh Saeed Ahmad ametoa wito wa kuanzishwa 'Umoja wa Mataifa ya Kiislamu' ili kutatua matatizo waliyonayo Waislamu duniani.
2014 Dec 07 , 09:23
Wafanya magendo ya binadamu wanawatumia vibaya wakimbizi Waislamu wanaokimbia mauaji na unyanyasaji wa kuchupa mipaka nchini Myanmar.
2014 Dec 01 , 10:36
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ege kilichoko katika mji wa Izmir nchini Uturuki amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kumzuia mwanafunzi aliyevaa hijabu ya Kiislamu kuingia darasani.
2014 Nov 30 , 11:11
Ayatullah Sheikh Issa Qassim Kiongozi mkubwa wa kidini nchini Bahrain ametoa wito kwa wananchi wa nchi hiyo kuendelea kusimama kidete na kukabiliana na changamoto kubwa zinazowakabili ikiwemo dhulma inayofanywa na utawala wa kifalme wa nchi hiyo wa Aal Khalifa.
2014 Nov 29 , 10:23
Magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIL) wameharibu misikiti kadhaa na Haram tukufu za Waislamu wa Sunni na Shia katika mkoa wa Salahuddin nchini Iraq.
2014 Nov 28 , 06:07
Kongamano la Kimataifa la ‘Hatari ya Misimamo Mikali Na Utakfiri Kwa Mtazamo wa Maulamaa wa Kiislamu’ lilianza jana hapa nchini Iran katika mji Mtakatifu wa Qum kusini mwa Tehran kwa kuhuduriwa na mamia ya maulamaa na wanafikra wa Kiislamu kutoka madhehebu ya Shia na Sunni.
2014 Nov 24 , 13:29
Waislamu nchini Kenya wamelalamikia vikali hatua ya serikali ya nchi hiyo kufunga misikiti kadhaa katika Kaunti ya Mombasa.
2014 Nov 23 , 11:36
Serikali ya Uturuki imetangaza kuanza mpango wa ujenzi wa misikiti katika vyuo vikuu vyote vya umma nchini humo.
2014 Nov 22 , 11:34
Rais Rajab Tayyib Erdogan amesema Bara Amerika lilivumbuliwa na Waislamu katika karne ya 12 Miladia, karibu karne tatu kabla ya Christopher Columbus kufika hapo.
2014 Nov 17 , 16:41
Kiongozi mwandamizi wa Baraza la Uhusiano wa Kiislamu nchini Marekani (CAIR) ameitaka Polisi ya Marekani FBI kuacha kufanya ujasusi ndani ya Misikiti nchini humo.
2014 Nov 15 , 20:33