Balozi na mwambata wa kiutamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Falme za Kiarabu siku ya Alkhamisi ijayo wanatazamiwa kushiriki kwenye maonyesho ya sanaa mjini Doha Qatar ambapo msanii mashuhuri wa Iran anatazamiwa kuonyesha kazi zake za uandishi wa Qur'ani kwa kutumia mkono.
2012 Jul 17 , 12:44
Vikao maalumu vya Qur'ani ambavyo vimepangwa kufanyika katika mwezi wa Ramadhani chini ya anwani ya 'Kutafakari kwenye Qur'ani; Njia ya Maisha' vitafanyika katika Kituo cha Kiislamu mjini London Uingereza.
2012 Jul 16 , 23:50
Mbinu za ufundishaji Qur'ani Tukufu na maarifa ya Kiislamu zitafundishwa katika Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali (as) mjini Vienna, mji mkuu wa Austria.
2012 Jul 16 , 23:48
Taasisi ya Masuala ya Kidini ya Uturuki limezindua Tovuti ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya kutumiwa na Waislamu wa nchi hiyo wanaojishughulisha na masuala ya tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kituruki.
2012 Jul 16 , 23:46
Mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu makhsusi katika mwezi wa Ramadhani yamepangwa kufanyika tarehe12 Agosti katika mji wa Montreal nchini Canada.
2012 Jul 15 , 12:09
Duru ya pili ya masomo ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu na kutadabari katika aya za kitabu hicho itaanza kesho Jumatatu kwa usimamizi wa Idara ya Utalii ya Dubai.
2012 Jul 15 , 12:09
Hafidhi wa Qur'ani Tukufu mwenye umri wa miaka 86 ambaye amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima Niyazi Ozcelik ameenziwa na kituo cha kidini cha mkoa wa Düzce nchini Uturuki.
2012 Jul 14 , 17:58
Mashindano ya taifa ya hifdhi na kiraa ya Qur’ani Tukufu yamepangwa kufanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Uingereza.
2012 Jul 14 , 14:37
Kongamano la Utatuzi wa Migogoro ya Kijamii kwa Mtazamo wa Qur’ani limepangwa kufanyika katika Taasisi ya Qur’ani Tukufu ya mji wa Lucknow katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India.
2012 Jul 14 , 14:37
Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yatafunguliwa rasmi Julai 15 katika sherehe itakayohudhuriwa na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2012 Jul 14 , 11:18
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Pew ya Marekani umebaini kuwa licha ya kupita mwaka mmoja sasa tangu baada ya kuanza mwamko wa Kiislamu, harakati za demokrasia bado inapendwa na kukubaliwa na watu wengi katika nchi sita za Waislamu zilizokumbwa na mapinduzi ya wananchi na kwanba watu wengi katika nchi hizo wanataka sheria zinazotokana na mafundisho ya Qur’ani.
2012 Jul 11 , 15:21
Hivi sasa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio inayoongoza katika harakati za Qur’ani katika ulimwengu wa Kiislamu, amesema mbunge mmoja wa Iran.
2012 Jul 11 , 14:07
Washiriki katika mashindano ya hifdhi ya Qur’ani Tukufu makhsusi kwa ajili ya wasichana huko Dubai wameanza kujiandikisha leo Jumanne.
2012 Jul 10 , 17:36