IQNA

Hali ya Waislamu Nigeria

Msikiti wavamiwa Nigeria, waumini 19 watekwa nyara

15:50 - December 06, 2022
Habari ID: 3476205
TEHRAN (IQNA) Watu wenye silaha wameshambulia msikiti mmoja kaskazini mwa Nigeria na kuwateka nyara watu 19 huku visa vya utekaji nyara vikiongezeka nchini humo.
Kwa mujibu wa vyombo rasmi vya serikali, tangu mwishoni mwa mwaka 2020 hadi sasa, maeneo ya kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria yamekuwa yakishuhudia ongezeko la mashambulizi ya silaha. Vitendo vya utekaji nyara wa halaiki na aina zingine za uhalifu wa utumiaji nguvu vimeongezeka mno katika maeneo hayo huku serikali ikishindwa kurejesha nidhamu na utawala wa sheria.
Gambo Isa, msemaji wa polisi ya jimbo la Katsina nchini Nigeria amesema, watu waliobeba silaha walishambulia msikiti wa kijiji kimoja katika eneo la Fontwa wakati wa Sala ya Isha hapo jana na baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi imamu wa msikiti huo na mtu mmoja mwingine waliwateka nyara waumini 19 msikitini humo.

Msemaji huyo wa polisi ya mkoa wa Katsina ameongezea kwa kusema: vikosi vya usalama viliwaandama washambuliaji hao na kufanikiwa kuwakomboa watu sita; na juhudi za kuwakomboa waumini wengine waliotekwa nyara zingali zinaendelea.

Miezi michache iliyopita, vikosi vya majeshi ya Chad, Cameroon, Nigeria na Niger vilifanya shambulio lililoratibiwa kwa pamoja na nchi hizo nne kwa lengo la kuliangamiza kundi la Boko Haram na makundi mengine ya kigaidi yanayoendesha harakati zao katika eneo la kandokando ya Ziwa Chad.
3481542
Kishikizo: nigeria waislamu
captcha