IQNA

Haram ya Hadhrat Abdul Adhim Hassani

TEHRAN (IQNA)- Tarehe Nne Mfunguo Saba Rabiuthani 1444 Hijria SAW tarehe 30 Oktoba 2022 Milaadia ni kumbukumbu ya kuzaliwa Sayyid Abdul Adhim al Hassani aliyekuwa mmoja wa wajukuu wa Imam Hassan al Mujtaba AS huko katika mji wa Madina miaka 1271 iliyopita

Sayyid Abdul Adhim alikuwa mmoja kati ya shakhsia walioaminiwa na Imam al Hadi AS na alinukuu hadithi moja kwa moja kutoka kwa maimamu watukufu kama vile Ridha, Jawad na al Hadi AS. Sayyid Abdul Adhim alihamia Iran kutokana na pendekezo la Imam al Hadi AS  kwa ajili ya kuwaongoza Waislamu na akaishi katika mji wa Rei karibu na Tehran ya sasa. Sayyid Abdul Adhim aliuawa shahidi mwezi Shawwal mwaka 250 Hijria. Hapa chini ni picha za Kaburi (Haram) la mtukufu huyo ambalo liko katika eneo la Rei na ni miongoni mwa maeneo yanayotembelewa na Waislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani.

.