IQNA

Maktaba ya Amir Al-Mu’minin huko Najaf

NAJAF (IQNA) - Maktaba ya umma ya Imam Amir al-Mu'minin ni maktaba kuu katika mji mtakatifu wa Iraq wa Najaf.

Maktaba hii  ilianzishwa na marehemu mwanazuoni wa Kiislamu Allamah Amini mwaka wa 1954, na inajumuisha sehemu mbalimbali na inasimamiwa na bodi ya wadhamini.
Katika maktaba hii maarufu kuna maelfu ya vitabu vya kihistoria na vya kisasa katika nyanja mbalimbali kama vile Uislamu, Quran, hisabati, na fizikia. Maktaba hiyo hutembelewa zaidi na wanafunzi wa vyuo vya Kiislamu kutoka Iran na Iraq.
Allamah Amini (1902-1970) alikuwa mwanazuoni wa ngazi za juu wa madhehebu ya Shia katika karne ya 20 na anajulikana sana kwa kitabu chake cha juzuu 11 “Al-Ghadir”.
Amezikwa karibu na maktaba.

Kishikizo: maktaba