IQNA

Hujjatul Islam Hamid Shahriari

Matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu yamekita mizizi katika masuala ya kisiasa

21:54 - September 23, 2022
Habari ID: 3475827
TEHRAN (IQNA) – Msomi mwandamizi wa Kiislamu nchini Iran anasema matatizo mengi ya ulimwengu wa Kiislamu yanatokana na masuala ya kisiasa kati ya nchi.

Hujjatul Islam Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukuruisha Madhehebu za Kiislamu ameyasema hayo katika mkutano wake Adel Bour, mwakilishi wa masuala ya kidini ya Uturuki nchini Iran.

"Kwa kweli kile ambacho wanasiasa wanakifuata katika nyanja ya kidiplomasia kinasababisha matatizo katika ulimwengu wa Uislamu," Shahriari alisema.

Aidha amesisitiza kuwa iwapo wasomi wa kidini watafuata mfumo thabiti, basi wanaweza kuchukua jukumu katika uwanja wa kisiasa.

"Dini kamwe haifuatii vita na ugaidi. Dini zote zinaheshimu maisha ya mwanadamu. Qur’ani Tukufu inasema kwamba anayemuua mtu mmoja kwa ni kana kwamba ameua ubinadamu wote."

Qur'ani Tukufu inalenga kuleta amani amani duniani, alisema, akitoa wito kwa wanazuoni kueleza masuala mbalimbali ya suala hili kwa jamii.

Kumekuwa na tafsiri mbalimbali za dini katika historia, alisema, akiongeza kuwa hii haipaswi kusababisha migogoro na iwapo  hifilafu za  kidini zitasababisha ugaidi na ukufurishaji, basi ni kinyume na kanuni za Kiislamu.

Shahriari pia alikosoa namna vyombo vya habari  vinavyotumiwa kuvunjia heshima itikadi za wengine huku akitoa wito wa kudumishwa  nidhamu wakati wa kutokubaliana.

Kwa upande wake, afisa huyo wa Uturuki aliashiria ulazima wa ukaribu kati ya madhehebu za Kiislamu.

3480599

captcha