IQNA

Hafla ya Tashtgozari yafanyika Tehran

TEHRAN (IQNA)- Hafla ya ‘Tashtgozari’ ya kuashiria kuanza maombolezo ya mwezi wa Muharram imefanyika mjini Tehran, Iran katika Husseiniya ya Chuo Kikuu cha Imam Hussein Mujtaba na Msikiti wa Wardebili.

Tashtogozari ni moja ya mijimuiko ya kale ya Wairani hasa wa maenei ya kaskazini magharibi ambayo hufanyika kabla ya kuanza mwezi wa Muharram.

Katika mjumuiko huu, waombolezaji hubeba bakuli za maji kama nembo ya maji ya Mto Furati (Euphrates); haya ni maji ambayo Imam Hussein AS na familia yake walinyimwa maji na maadui.

Kwa mujibu wa riwaya, wakati Al Hurr ibn Yazid alifunga njia ya Imam Hussein AS karibu na Karbala, Imam Hussein AS aliona kiu na uchovu wake na jeshi lake na hivyo akawaagiza masahaba zake wajaze maji katika mabakuli ili wanajeshi na wanyama wawezi kunywa.