IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Shahidi Mustafa Badruddin alikabiliana na Wazayuni na magaidi wakufurishaji

22:26 - May 20, 2022
Habari ID: 3475271
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amehutubu kwa munasaba wa kukumbuka kuuawa shahidi Sayyid Mustafa Badruddin na kusema kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kulikuwa ni pigo kwa nchi za Kiarabu na mataifa yote ya eneo.

Shahid Badruddin alikuwa kamanda wa kijeshi wa Hizbullah ambaye aliuawa shahidi Mei 13 katika hujuma ya magaidi karibu na uwanja wa ndege wa kijehsi wa Damascus, mji mkuu wa Syria.

Akizungumza kwa munasaba wa mwaka wa sita kuuawa shahidi Sayyid Mustafa Badruddin, maarufu kwa lakabu ya Dhu al-Faqar, Sayyid Nasrallah amesema:"Sayyid Badruddin alikuwa kijana aliyepitisha umri wake katika kukabiliana na mustakbirina na kupambana na Uzayuni na magaidi wakufurishaji"

Katibu Mkuu wa Hizbullah aidha amewashukuru watu wa Lebanon kwa kushiriki katika uchaguzi wa bunge hasa Walebanon waishio nje ya nchi na kusema yamkini waliopigia kura Hizbullah wakapata matatizo lakini pamoja na hayo wamepiga kura na hivyo wanapaswa kushukuriwa.

Sayyid Nasrallah ameashiria kadhia ya Palestina na kusema taifa la Palestina  halisubiri tena msaada wa nchi za Kiarabu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu au Umoja wa Mataifa na katika katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, aghalabu ya Wapalestina wanaamini kuwa njia pekee ya ukombozi ni mapambano ya silaha.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameendelea kusema kuwa, ilitazamiwa kuwa nchi za Kiarabu zingeisiadia Palestina ikombolewe lakini badala ya hilo Wazayuni wameteka na kukalia kwa mabavu mji wa Quds, Ukingo wa Magharibi, Miinuko ya Golan, Mashamba ya Shebaa na Eneo la Sinai.

Kiongozi wa Hizbullah amesema Lebaon pia ingekumbwa na maafa kama ya Palestina na iwapo Hizbullah haingekuwepo Walebanon wangekumbwa na maaafa makubwa.

Sayyid Nasrallah amezikosoa nchi za Kiarabu ambazo zimeanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa hakupaswi kuwa na dhana kuwa nchi za Kiarbau zitaisiadia Lebanon. Amesema wakati nchi za Kiarabu zilipokuwa na msjhikamano hazikuweza kuikomboa Palestina hivyo leo pia ndio kabisa haziwezi kuikomboa Palestina. Amesema hata hazikusaidia kukomboa maeneo ya Lebanon yaliyokuwa yanakaliwa kwa mabavu bali ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Syria pekee ndizo zilizounga mkono Lebanon.

4058399

captcha