IQNA

Maelfu ya Waislamu washiriki sala ya Ijumaa Msikiti wa Al Aqsa

21:49 - May 20, 2022
Habari ID: 3475270
TEHRAN (IQNA)- Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) pamoja na kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ulijaribu kuwazuia waumini kufika katika eneo hilo takatifu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina, maelfu ya Wapalestina walifanikiwa kusali Sala Ijumaa katika Msikiti wa Al Aqsa ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni unaokali Quds Tukufu kwa mabavu waliweka vituo vya upekuzi kuelekea msikiti wa Al Aqsa na kuwazuia Wapalestina kufika katika Msikiti wa Al Aqsa.

Wapalestina walianza kuingia Msikiti wa Al Aqsa mapema Ijumaa kujitayarisha kwa ajili ya Sala ya Ijumaa.

Makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina yametangaza kuwa Wapalestina watasimama kidete kukabiliana na jinai za Israel sambamba na kuuhami mji wa Quds na Msikiti wa Al Aqsa.

 

Hayo yanajiri wakati ambao wiki hii Utawala wa Kizayuni ulimpiga marufuku kwa miezi minne Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa Sheikh Ikrima Sabri kutokanyaga katika eneo la msikiti huo kutokana na kile ulichokitaja kuwa hatua za Sheikh Sabri za kuuteteta msikiti huo.

Msikiti wa al Aqsa ambao ni nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu wa Palestina huko Quds au Baitul Muqadas umekuwa ukilengwa na hujuma na mashambulizi haribifu ya utawala ghasibu wa Israel. 

Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa amejibu haraka kitendo hicho cha uhasama na chuki cha utawala wa Kizayuni dhidi yake.  Sheikh Sabri amesema kuhusiana na hilo kwamba na hapa ninamkukuu: "Nitaendelea kuutetea Msikiti wa al Aqsa na wala sitakaa kimya wala kusalimu amri bali nitaendelea kuutetea msikiti huo hadi mwisho wa maisha yangu', mwisho wa kunukuu.  

Sheikh Ikrima Sabri aidha ameashiria namna walowezi wa Kizayuni pekee yao wasivyo na uthubutu wa kuuvamia na kuuhujumu Msikiti wa al Aqsa bila ya msaada wa wanajeshi wa Israel na kusisitiza kuwa; tunaapsa kuwa makini na macho dhidi ya njama na hila za maghasibi wa Kizayuni."  

4058360

Kishikizo: aqsa quds tukufu sabri
captcha