Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh Ahmed el Tayyib atafanya ziara rasmi nchini Iraq mwezi Oktoba. Sheikh Mkuu wa Al Azhar ameitaja Iraq kuwa ‘nchi azizi’ huku akisema kuna nukta nyingi za paoja baina ya Misri na Iraq.
Akiwa safarini Iraq atatembelea mji mkuu wa Baghdad, mji wa Erbil katika eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan, mji wa Mosul na halikadhalika mji mtakatifu wa Najaf.
Ubalozi wa Iraq mjini Cairo umetangaza kuwa kutakuwa ni shughuli kadhaa muhimu wakati Sheikhe Mkuu wa Al Azhar atakapotembelea Iraq.