IQNA

Mwanajudo wa Sudan naye akataaa kucheza na Muisraeli katika Michezo ya Olimpiki 2020

20:08 - July 26, 2021
Habari ID: 3474130
TEHRAN (IQNA) - Mwanamichezo wa mchezo wa Judo kutoka Sudan Mohamed Abdalrasool amekuwa mwamichezo wa pili kukataa kucheza na Muisraeli Tohar Butbul katika michezo ya Olimpiki 2020 ya Tokyo.

Maafisa wa Olimpiki wanasema Abdalrasool hakujitokeza katika mchuano dhidi ya Butbul Jumatatu. Wakuu wa Sudan hawakutoa taarifa punde baada ya tukio hilo.

Mualgeria Fethi Nourine naye pia alikataka kucheza na Muisraeli huyo huyo na hatua yake hiyo ya kishujaa imepelekea asimamishwa kwa muda na Shirikisho la Kimataifa la Judo. Mwaka 2019 Nourine pia alikataa kucheza na Butbul.

Mohamed Abdalrasool  amechukua hatua hiyo ya kishujaa ya kukataa kucheza na mwakilishi wa utawala haramu wa Israel ambao unakoloni ardhi za Palestina katika hali ambayo nchi yake, Sudan imeanzisha uhusiano na utawala huo dhalimu. Hatua hiyo ni ishara ya wazi kuwa wannachi waliowengi Sudan hawaafiki uamuzi watawala wa nchi hiyo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mwaka jana Shirikisho la Kimataifa la Judo lipiga marufuku Shirikilisho la Judo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa muda wa miaka minne  baada ya wanajudo wa Iran kukataa kucheza na Muisraeli. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiitambui Israel kama nchi.

3475333

captcha