IQNA

Sheikh Isa Qassim akosoa utawala wa Bahrain kwa kukiuka haki za binadamu

14:51 - July 17, 2021
Habari ID: 3474109
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi mkuu wa Kiislamu nchini Bahrain amewataka watawala wa nchi hiyo kuwaachilia huru mara moja wafungwa wote wa kisiasa nchini humo.

Katika taarifa kuopitia tovuti ya Bahrain Mirror, Sheikh Isa Qassim amekosoa vikali ukiukwaji wa haki za binadamu unaotekelezwa na ufalme wa Bahrain na kusema haiwezekani kusubiri bunge liitishe kikao kujadili kadhia ya wafungwa.

Amesisitiza kuwa ili kuwepo uhusiano mzuri baina ya wananchi na serikali, lazima kuwepo na sheria za uchaguzi zenye kuzingatia usawa na sheria hizo zinapaswa kuungwa mkono na serikali pamoja na wapinzani.

Mwamako wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 2011. Mwamko huu ni tofauti na harakati zingine za mwamko katika uliwengu wa Kiarabu ukiwemo mwamko uliopelekea kuangushwa Zine El Abidine Ben Ali wa Tunisia au Husni Mubarak wa Misri. Tofauti ya mwamko wa watu wa Bahrain ni kuwa, nchi hiyo inapakana na Saudi Arabia ambayo ni mpinzani na adui mkubwa zaidi wa mwamko na mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu.

Kwa msingi huo, mwezi mmoja baada ya kuanza mwamko wa Februari 14, utawala wa Saudia ulituma wanajeshi wake Bahrain kwa lengo la kuwakandamiza raia wa nchi hiyo. Askari hao vamizi wa Saudia waliingia Bahrain katika fremu ya 'Ngao ya Kisiwa' ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi. 'Ngao ya Kisiwa' ni mapatano ya ushirikiano wa kijeshi wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kukabiliana na hujuma ya kigeni.

Hivi sasa ukiwa ni mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa watu wa Bahrain, wanajeshi wa Saudia na pia wale wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) bado wako nchini Bahrain na wanashirikiana na askari waliokodiwa wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa katika kuwakandamiza wananchi ambao wamekuwa wakiandamana kupigania mageuzi hasa ya kutaka kuwepo utawala unaochaguliwa moja kwa moja na wananchi.

3475257

captcha