IQNA

Jeshi la Yemen lapata mafanikio katika oparesheni ya Al-Nasr Al-Mubin dhidi ya Saudia na magaidi

21:40 - July 16, 2021
Habari ID: 3474104
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Yemen likishirikiana na Kamati za Kujitolea za Wananchi limeweza kutekeleza kwa mafanikio oparesheni ya Al-Nasr Al-Mubin katika mkoa wa Al-Baidha (Al Bayda).

Oparesheni ya Al Nasr al Mubin ina umuhimu mkubwa na vigezo kadhaa.

Kigezo cha kwanza katika oparesheni hii ni kuwa imetekelezwa dhidi ya magaidi wakufurushaji. Katika hali ambayo muungano vamizi wa Saudia na waitifaki wake wamekuwa wakidai kuwa eti harakati ya Ansarullah ya Yemen ni kundi la kigaidi, harakati hiyo imeweza kuunda Serikali ya Uwokozi wa Kitaifa yenye makao yake katika mji mkuu Sanaa na iko mstari wa mbele katika kupambamba na magaidi. Oparesheni ya Al Nasr Al Mubin ilikuwa dhidi ya magaidi wa ISIS na Al Qaeda  ambapo makundi hayo mawili ya kigaidi yamepata hasara kubwa sana.

Kigezo cha pili katika oparesheni hiyo ni kuwa imefanyika katika mkoa ulio kati mwa Yemen. Maeneo ya Al-Soma, Al-Zahir katika mkoa wa Al Baidha yalikuwa kitovu cha oparehsehni hiyo. Nukt hii inaonyesha kuwa Jeshi la Yemen likishirikiana na Kamati za Kujitolea za Wananchi limeweza kueneza wigo wa oparesheni zake.

سخنگوی نیرو‌های مسلح یمن جزئیات عملیات النصر المبین را تشریح کرد

Na kigezo cha tatu katika oparesheni hiyo ni kuwa imefanyika katika muda mfupi sana. Akizungumza Alhamisi, Msemaji wa Jeshi la Yemen Yahya Saree amesema oparesheni ya Al Nasr Al Mubin ambayo imefanyika wiki hii imechukua muda wa masaa 72 na nukta hii inaonyesha kuwa, Jeshi la Yemen likishirikiana na Kamati za Kujitolea za Wananchi linaweza kutekeleza oparesheni za haraka na kwa mafanikio.

Oparesheni ya Al Nasr Al Mubin pia ina nukta kadhaa muhimu

Katika oparesheni hii mshikamano baina ya Jeshi la Yemen na Kamati za Kujitolea za Wananchi umeweza kubainika wazi katika mkoa wa Al Baidha. Mshikamano huu umeweza kuwa na nafasi muhimu katika mafanikio ya Jeshi la Yemen.

Ni kwa msingi huo ndio Yahya Saree akatangaza kuwa,  wananchi wamekuwa na nafasi kubwa katika mkoa wa Al Baidha na hivyo ametoa shukrani zake za dhati kwa mchango wao mkubwa.  Msaada huo wa wananchi ndio umepelekea muungano wa Saudia na magadi wa Al Qaeda usiweze kufikia malengo yake.

Nukta nyingine muhimu katika oparesheni hii ni kuwa imebainika wazi kuwa kuna ushurikiano wa karibu baina ya magaidi na muungano vamizi unaoongozwa na Saudia ambao ulianzisha vita dhidi ya Yemen mnamo Machi 2015. Serikali ya Uwokozi wa Kitaifa ya Yemen imechapisha taswira zinaoashiria ushirikiano huo wa karibuni baina ya Saudia na magaidi. Ufichuzi wa kashfa hiyo umewakasirisha sana Wasaudi na kuilazimu televisheni ya Al Arabiya ya utawala wa Riyadh kudai kuwa eti taswira hizo zinazoonyesha magaidi wa Al Qaeda wakipigana bega kwa bega na askari wa Saudia si za kweli.

سخنگوی نیرو‌های مسلح یمن جزئیات عملیات «نصر المبین» را تشریح کرد

Ni wazi kuwa, muungano vamizi wa Saudia unaoshirikiana na magaidi umepata pigo kubwa katika medani ya vita na sasa kunashuhudiwa mabadiliko katika mlingano wa nguvu Yemen. Saudia inajaribu kuwatumia magaidi wa Al Qaeda na ISIS kuzuia Jeshi la Yemen na Kamati za kujitolea za Wananchi kusona mbele kwa kasi. Nukta hii inaashiria wazi kuwa, Serekali ya Uwokozi wa Kitaifa ya Yemen ina azma na irada ya kukomboa maeneo yote ya nchi hiyo ambayo yanakaliwa kwa mabavu na hivyo muungano vamizi wa Saudia utapata pigo kubwa kwani umeshindwa kukabiliana na vikosi vya Serikali ya Uwokozi wa Kitaifa ya Yemen.

3984346

captcha