IQNA

Qiraa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikh Mutawalii Abdul Aal ya Surah An-Naziat +Video

22:00 - July 29, 2020
Habari ID: 3473013
TEHRAN (IQNA)- Kuna idadi kubwa ya qiraa za qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Sayyid Mutawalli Abdul Aal aliyeaga dunia mwaka 2015.

Moja kati ya qiraa zake mashuhuri ni hii iliyo hapa chini ambapo anaseoma aya za Sura An-Naziat ya  79 ya Qur’ani Tukufu kwa pumzi moja.

Katika klipu hii anasoma aya za 26 na 27 za Sura An-Naziat  zisemazo: “Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!.”

Ustadh Mutawalii Abdul Aal alizaliwa Aprili 1947 katika familia yenye kuzingatia dini nchini Misri na aliweza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka 12. Baadaye alianza qiraa ya Qur’ani kwa kuiga mtindao ya usomaji wa Sheikh Abdulbasi na Sheikh Mustafa Ismail na hatimaye akaibua mtindo wake.

Alifanikiwa kutumbelea nchi mbali mbali duniani kama qarii na pia kama jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani.

Aliaga dunia Julai 16 akiwa na umri wa miaka 68.

3913191

captcha