IQNA

Hizbullah: Madai ya Israel kuhusu mapigano mpakani ni njama ya kupata ushindi bandia

21:29 - July 28, 2020
Habari ID: 3473008
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa ikikanusha madai ya vyombo vya habari vya Kizayuni kuhusu oparesheni ya kujipenyeza wapiganaji wake Israel.

Jeshi la utawala wa Kizayuni  jana Julai 27 likashambulia miinuko ya Kafr Shuba ya Lebanon na mashamba yanayokaliwa kwa mabavu ya Shebaa. Sambamba na mashambulio hayo, vyombo vya habari vilianzisha propaganda dhidi ya Hizbullah na baadhi ya vyombo vya habari vya Kizayuni vikatangaza kuwa, Hizbullah imetekeleza oparesheni ya kujipenyeza hadi ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) ambapo Israel nayo ilijibu mapigo na kuwaua shahidi au kuwajeruhi wapiganaji wa Hizbullah.

Baada ya propagnada hizo, Hizbullah ilitoa taarifa ya haraka ikikanusha madai hayo ya vyombo vya habari vya Kizayuni kuhusu oparesheni hiyo ya kujipenyeza Israel na kuuawa shahidi au kujeruhiwa wapiganaji wake. Hizbullah imesema propaganda hizo zilikuwa katika jitihada za utawala wa Kizayuni za kubuni ushindi bandia.

Taarifa hiyo kwa upande mmoja ilionyesha kushindwa utawala wa Kizayuni katika vita vya kisaikolojia dhidi ya Hizbullah na kwa upande mwingine imeendelea kudumisha tishio la Hizbullah dhidi ya utawala wa Kizayuni kuhusu kulipiza kisasi cha kuuawa shahidi Ali Kamel Muhsin. Hizbullah imetangaza bayana kuwa,  bila shaka muqawama  utatoa jibu kali la kuuawa shahidi mmoja wa wapiganaji wake na pia kushmabuliwa kwa mabomu jana nyumba ya raia katika kijiji cha al Habariya katika mpaka wa Lebanon.

3472110

captcha