IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Marekani inapinga demokrasia nchini Iraq

11:22 - April 07, 2019
Habari ID: 3471903
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Marekani inapinga mchakato wa demokrasia nchini Iraq.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ameyasema hayo Jumamosi mjini Tehran aliponana na Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul Mahdi hapa mjini Tehran na kusisitizia wajibu wa kuhakikisha kwamba Marekani inaondoa wanajeshi wake haraka iwezekanayo huko Iraq.
Amesema kuwa, katika nchi yoyote ambayo Wamarekani wamekuwa na wanajeshi wao kwa muda mrefu, mchakato wa kuwatoa nchini humo unakuwa mgumu.
Vile vile amesema kuwa, wananchi wa mataifa mawili ya Iran na Iraq wana historia ndefu sana ya ushirikiano wa kiitikadi, kiutamadui na kihistoria na kusisitiza kuwa, uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq unapindukia uhusiano wa nchi mbili jirani na kwamba serikali na taifa la Iran linayahesabu maendeleo na manufaa ya Iraq kuwa ni kwa manufaa yake.
Hata hivyo amesema, Marekani inaona machafuko na hatari za kiusalama za Iraq kuwa ni kwa manufaa yake, tofauti kabisa na madai ya dhahiri yanayotolewa na viongozi wa Washington. Hivyo kuna haja kwa taifa la Iraq kufanya haraka kuwafukuza wanajeshi wa Marekani nchini mwao.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amebainisha kuwa, Marekani na vibaraka wake katika eneo wanapinga mchakato wa hivi sasa wa kidemokrasia nchini Iraq wakiamini kuwa mchakato huo utapingana na maslahi yao.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, serikali ya Iraq, Bunge na wanaharakati wa kisiasa wa hivi sasa nchini humo hawakufadhilishwa na wala hawaungwi mkono na Marekani, na kwa msingi huo Washington inapanga njama za kuwaondoa katika uga wa kisiasa nchini Iraq.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul Mahdi amepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi yake na Iran, na kusisitiza kuwa Baghdad katu haitaungana wala kushirikiana na Marekani katika kuiwekea vikwazo Tehran.

3468234

captcha