Nakala hiyo ya kipekee ya Qur’ani ni kati ya vitu vya umbo dogo vinavyoonyeshao katika maonyesho hayo ya kipkee.
Nakala hiyo ndogo ya Qur’ani iliandikwa kwa mkono na Necati Korkmaz ambaye ni Mturuki pekee mwenye uwezo wa kuandika kaligrafia kwa mtindo wa Gubari.
Nakala hiyo ya Qur’ani imetajwa kuwa una ukubwa wa chini ya sentimeta moja na iliandikwa katika kipindi cha miaka mitatu.
Necati Korkmaz anasema aghalabu alifanya kazi hiyo ya kipekee wakati wa usiku. Aidha anasema amewahi kuandika majina 99 ya Allah katika ndengu moja na Bismillahi Ar Rhamani Ar Rahim katika unywele. Uandishi huo unatumia kalamu maalumu kwa kutegemea hadubini mikroskopu.