IQNA

Iran Kuisaidia Senegal Kuimarisha Shule za Qur’ani

11:41 - July 10, 2018
Habari ID: 3471589
TEHRAN (IQNA)-Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Senegal kimetangaza utayarifu wake katika kuisaidia nchi hiyo kuimarisha shule au Madrassah za Qur’ani Tukufu.

Hayo yamebainika katika mkutano baina yaviongozi wa Kiislamu katika miji ya Touba na Kaolack na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Senegal Mheshimiwa Ainollah Qashqavi aliyekuwa ameandamana  na Mwambata wa Utamaduni wa Iran Sayyid Hassam Esmati.

Katika mikutano hiyo, balozi wa Iran amebainisha azma ya Iran kuimarisha ushirikiano wake na Senegal katika nyanja zote. Kwa upande wake, Sayyid Esmati amesisitiza kuwa Kituo cha Utamaduni cha Iran kiko tayari kuimarisha uhshirikiano na Madrassah na taasisi za Qur’ani katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Kwa upande wao, viongozi wa Kiislamu katika miji ya Touba na Kaolack wameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa nafasi yake chanya katika ulimwengu wa Kiislamu huku wakitoa wito wa kuimarishwa uhusiano wa Senegal na Iran.

Karibu asilimia 93 ya watu wote nchini Senegal ni Waislamu na aghalabu ni Masufi wenye kufuata madhehebu ya Imam Malik.

3728281

captcha