Bi. Ferdows Awadi, mwanachama wa Muungano wa Utawala wa Sheria katika Bunge la Iraq, ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua za kuzima njama hiyo.
Ametahadharisha kuwa, iwapo serikali haitachukua hatua za dharura, basi baadhi ya maeneo ya Iraq yataanguka mikononi mwa magaidi.
"Hivi sasa kuna njama zinazotekelezwa na Marekani kuhuisha kundi la kigaidi la ISIS ili kuliwezesha kukalia kwa mabavu baadhi ya maeneo ya kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo," amebaini mbunge huyo.
Aidha Awadi amefichua kuwa Wamarekani wanalenga kuitumbukiza Iraq katika vita vipya vya ndani sambamba na kuibua matatizo ya kiuchumi nchini humo.
Ametoa wito kwa Wairaqi kukabiliana na njama hiyo, ambayo pia inalenga wapiganaji wa kundi la kujitolea la wananchi, Al Hashd al Shaabi.
Mwezi Disemba mwaka 2017, Waziri Mkuu wa Iraq Haider al Abadi alitangaza kumalizika oparesheni ya miaka mitatu ya wanajeshi wa nchi hiyo kuwatimua magaidi wa ISIS. Oparesheni hiyo ilifanikiwa kwa msaada wa wapiganaji wa Al Hashd al Shaabi.