IQNA

Mkutano wa Idhaa za Qur'ani Duniani kufanyika Cairo

22:04 - January 23, 2018
Habari ID: 3471368
TEHRAN (IQNA)-Mkutano wa Nne wa Idhaa za Qur'ani duniani umepangwa kufanyika mjini Cairo, Misri kuanzua Januari 28-30.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo umeandaliwa na Jumuiya ya Kimatiafa ya Utangazaji inayofungamana na Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC. Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirkiano na Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO) pamoja na Jumuiya ya Kitaifa ya Vyombo vya Habari Misri.

Kikao hicho kinalenga kuimarisha nafasi na hadhi ya Idhaa au Radio  za Qur'ani  duniani na pia kujadili mbinu za kuwavutia vijana katika Uislamu na namna na kukabiliana na wimbi la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika vyombo vya habari vya nchi zisizo za Kiislamu.

Kikao hicho pia linalenga kujadili changamoto za kiufundi katika Idhaa za Qur'ani duniani huku washiriki wakijadili njia za kuimarisha uhusiano na kubadilishana vipindi.

3684526/

captcha