IQNA

Iran kuandaa mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi

12:59 - January 22, 2018
Habari ID: 3471365
TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapanga kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanafunzi Waislamu katika mwezi wa Aprili sambamba na Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran.

Akizungumza na Radio ya Qur'ani ya Iran, Hujjatul Islam Seyed Mustafa Husseini, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Wakfu la Iran  amesema, sawa na mwaka 2017, Mashindano ya Kiamtaifa ya Qur'an ya Iran mwaka huu, mbali na yake ya kawaida, pia kwa wakati moja yatajumuisha mashindano ya kimataifa ya Qur'ani maalumu kwa wanawake, wanafunzi wa vyuo vya kidini na ya wale wenye ulemavu wa macho.

Mashindano hayo yamepangwa kufanyika Aprili 19-26 mwaka 2018, kwa mujibu wa matangazo ya kamati andalizi.

Hujjatul Islam Hussein amesema Duru ya Sita ya Mashindano ya Kimataifa ya Wanafunzi Waislamu pia imepangwa kufanyika  mwezi Aprili pamoja na mashindano hayo mengine lakini uamuzi wa mwisho bado haujachukuliwa.

Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) imekuwa ikiandaa mashindano ya Qur’ani ya wanafunzi Waislamu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

3683695

captcha