IQNA

Daktari wa watoto ambaye ni qarii maarufu wa Qur'ani Misri

8:34 - October 19, 2017
Habari ID: 3471222
TEHRAN (IQNA)-Daktari Ahmed Ahmed Nuaina ni Qarii mashuhuri wa Qur'ani Misri na anatambuliwa kuwa miongoni wasomaji bora wa Qur'ani nchini humo.

Yeye ni daktari bingwa wa watoto na ana umri wa 63 na alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Matubas katika jimbo la Kafr El Sheikh. Anasema alianza kujifunza Qur'ani katika Madrassa akiwa na umri wa miaka mitatu. Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka minane na alienda kujifunza kanuni za Tajweed na Qiraa ya Qur'ani Tukufu.

Akiwa katika chuo kikuu, aliweza kupata umahiri wa kusoma Qur'ani kwa mbinu 10 tafauti na mwaka 1970 aliteuliwa rasmi kuwa Qarii au msomaji wa Qur'ani katika radio na televisheni ya kitaifa Misri.

Daktari Nuaina ameiga mbinu za usomaji Qur'ani za wasomaji mashuhuri kama vile Sheikh Abdul Basit Abdul Samad, Sheikh Abolainain Shoaisha, Sheikh Minshawi na Sheikh Hisri. Lakini aliyekuwa na taathira zaidi katika usomaji wake ni Sheikh Mustafa Ismail.

Katika mahojiano na jarida la kila wiki la Misri la al-Yawm al-Jadid, Daktari Nuaina anasema kazi yake kama daktari wa watoto haijamzuia kusoma Qur'ani. "Kila asubuhi baada ya sala ya alfajiri, mimi husoma Qur'ani. Aidha nikiwa njiani kuelekea katika hospitali hujishughulisha na usomaji Qur'ani na kwa uchache kila siku huwa ninasoma juzuu tano za Qur'ani."

Halikadhalika anasema mara kwa mara yeye husikiliza qiraa ya Qur'ani ya wasomaji bingwa Misri kama vile Minshawi, Mustafa Ismail, Ghalwash, Ahmed Amir na Bahtimi.

Daktari Sheikh Nuaina anasema amesafiri katika maeneo yote duniani kusoma Qur'ani na amechukua nafasi ya kwanza katika mashindano ya Qur'ani nchini India, Malaysia na Brunei.

Aidha amewahi kufika katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mara kadhaa katika jaji wa mashindano ya Qur'ani ya kimataifa.


Daktari wa watoto ambaye ni qarii maarufu wa Qur'ani Misri


Daktari wa watoto ambaye ni qarii maarufu wa Qur'ani Misri



Daktari wa watoto ambaye ni qarii maarufu wa Qur'ani Misri

3651647

captcha