IQNA

Nakala ya Qur'ani Tukufu iiyoandikwa na Mtumwa Mwafrika Marekani yaonyeshwa Beirut

12:47 - July 16, 2017
Habari ID: 3471069
TEHRAN (IQNA)-Nakala ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa na mtumwa Mwafrika nchini Marekani inaonyeshwa mjini Beirut Lebanon.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Rami al-Nimr, mfanya biashara Mpalestina anayeishi Beirut ameandaa maonyesho hayo ambayo pia yanajumuisha sanaa ya kaligrafia ya Kiarabu na nakala za zamani za Kiarabu.

Maoneysho hayo yalianza Aprili na yataendelea hadi Oktoba, amesema al-Nimr.

Katika maonyesho hayo kuna nakala ya Qur'ani iliyoandikwa na mtumwa Mwafrika nchini Marekani katika muongo wa 1740. Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, mtumwa huyo kijana alikuwa amenunuliwa na familia moja katika jimbo la Maryland . Alitoroka hapo na kisha na kukimbilia Pennsylvania ambako alikamatwa na kuswekwa jela alikoandika nakala hiyo ya Qur'ani, anasema Nimr. Mtumwa huyo pia alichora picha yake katika ukurrsa wa kwanza wa Msahafu huo. 

Inadokezwa kuwa nakala hiyo iliandikwa kwa mkono na Ayub bin Suleiman Diallo ambaye alikuwa amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu. Bin Suleiman alikuwa mtumwa kutoka Ufalme wa Futa Tora katika eneo la Afrika Magharibi ya leo. Kwa mujibu wa nyaraka za historia, Ayub bin Suleiman alikuwa Imamu wa msikiti kabla ya kutekwa nyara na Wazungu waliokuwa wakifanya biashara ya utumwa.


Nakla ya Qur'ani Tukufu Iliyoandikwa na Mtumwa Mwafrika Marekani yaonyeshwa Beirut

3619177

captcha